Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WAWILI KUJERUHIWA BAADA YA GALI KUPINDUKA MKOANI LINDI

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 



Na Abdulaziz Ahmed, Lindi
Watu wawili wamekufa na wawili kujeruhiwa baada ya gari waliyokuwa wanasafiria kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Michenga, wilaya ya Ruangwa Ruangwa mkoani Lindi.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi, ACP Renatha Mzinga alisema gari hiyo aina ya Toyota Rava4 yenye namba za usaji T574CWC.Iliyokuwa inaendeshwa na Mohamed Mchalaganya(27) iliacha njia na kupinduka katika barabara ya Ruangwa-Nanganga, ilitokea jana saa 11.30 jioni.

Kamanda Mzinga aliwataja waliokufa kwenye ajali hiyo kuwa ni Binasa Mapua(51) mkazi wa Tabata Dar-eS-salaam na Elizabeth Chipoleka(53),mkazi wa Yombo, Dar es salaam.

Kamanda Mzinga amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Mussa Mchalanganya na Rashid Mchalanganya ambaye ni mwanafunzi katika Chuo cha Usafirishaji (NIT), ambapo wote ni wakaazi wa Tabata, Dar es salaam. Dereva wa gari hilo ametiwa mbaroni na upelelezi unaendelea kujua chanzo hasa cha ajali hio.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>