Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Waokoaji wakijindaa kwenda katika eneo ilipotokea ajali ya mitumbwi iliyobeba harusi kutoka Kigoma mjini kwenda katika kijiji cha Kigalya kutafuta miili ya marehemu ambayo bado haijapatikana
Waokoaji toka vikosi mbalimbali wakiwemo wanajeshi wa JWTZ wakijiandaa kwenda kutafuta miili ambayo bado haijapatikana kutokana na jali ya mitumbwi katika kijiji cha kalalangabo.
Bibi harusi Mariamu Mduwa aliyenusurika katika ajali ya mitumbwi katika kijiji cha kalalangabo akiwa anaendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa wa Kigoma
Mariamu Mduwa baada ya mitumbwi miwili waliyokuwa wakisafiria kutoka kigoma mjini kwenda katika kijiji cha Kigalye kilichopo mwambao mwa ziwa Tanganyika kuzama ziwani.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Bibi harusi Mariamu Mduwa aliyenusurika katika ajali ya mitumbwi katika kijiji cha kalalangabo akiwa anaendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa wa Kigoma
Ndugu, jamaa na wapambe wa bwana na bibi harusi walionusurika katika ajali ya mtumbwi katika kijiji cha Kalalangabo wakiwa wanaendelea na matibabu katika hospita ya Mkoa wa Kigoma
Na Editha Karlo wa Kigoma
WATU sita wamekufa maji katika ziwa Tanganyika na wengine 11 kunusurika kifo akiwemo bwana harusi Shaaban Idd na bibi harusi
Tukio hilo limetokea leo saa nane na nusu mchana baada ya mitumbwi hiyo kupigwa wimbi kali na kuzama katika kijiji cha Kalalangabo wakati bwana harusi huyo akitoka kuoa katika eneo la mwandiga na kurudi nyumbani akiwa na ndugu na jamaa pamoja na wapambe.
Akiongea na Globu ya Jamii katika wodi namba 5 katika Hospital ya Mkoa wa Kigoma alipolazwa bibi harusi huyo alisema kuwa alishikwa na bumbuwazi sana baada ya tukio hilo kwani mpaka sasa bado hajielewi.
''Sikumbuki kitu kwani baada ya mtumbwi kuzama kila mtu alikuwa anahangaika kujiokoa na kifo.
"kwakweli mimi naona kama mkosi siku ya harusi yangu watu wanakufa ila namshukuru Mungu kwa kutunusuru na kifo na yote mimi nimemwachia Mungu''alisema bibi harusi huyo
Mwathirika mwingine aliyenusurika katika ajali hiyo Zabibu Issa alisema kuwa mitumbwi waliyokuwa wamepanda ilikuwa imejaza sana watu na mizigo ndiyo maana ilizidiwa uzito na kuzama baada ya kupigwa na wimbi.
''Safari ya kwenda kijijini kwetu lazima tupite njia za majini hakuna barabra kabisa sababu vijiji tunavyoishi vipo mwambao mwa ziwa Tanganyika kungekuwa na barabara tungepita barabrani''alisema Bi Zabibu Issa.
Naye muuguzi wa wodi namba tano walipolazwa majeruhi hao alisema kuwa majeruhi wote waliopo wodini hali zao zinaendelea vizuri na kwamba mpaka sasa wameshapokea jumla ya maiti sita.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma Jafari Mohamed akithibitisha hayo alisema kuwa mpaka sasa jumla ya watu 27 wameshaokolewa, na miili sita kuopolewa pamoja na walionusurika 11.
"Lakini bado inahofiwa kuwa kuna miili mingine zaidi ambao bado haijapatikana kwani mitumbwi hiyo inakadiriwa kuwa ilikuwa na watu zaidi ya sabini", alisema na kuongezea kuwa vikosi vya ukoaji kwa kushirikiana na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania vinaendelea na kazi ikiwa ni sambamba na kuchunguza chanzo cha tukio hilo.