Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

TAMASHA LA KUOMBEA TAIFA KUFANYIKA LEO OKTOBA 12-2014 LANDMARK HOTELI

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 

Dotto Mwaibale


NAIBU Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba leo ataongoza mamia ya wapenzi wa muziki wa injili kwenye tamasha la kuliombea taifa litakalo fanyika Hoteli ya Landmark Ubungo.



Akizungumza na mtandao wa  www, habari za jamii.com Dar es Salaam jana mratibu wa tamasha hilo ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za injili, Ibrahim Sanga alisema maandalizi yote ya tamasha hilo yamekamilika.


Sanga alisema tamasha hilo litakalokwenda sanjari na uzinduzi wa albamu ya Mungu ni Mwema na kuwa litaanza saa 7 mchana hadi saa 12 jioni.


“Tumejianda  vizuri kwa tamasha hili  ambalo litahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na dini na kuwa  miongoni mwa waimbaji watakaoimba katika tamasha hilo ni Mbunge wa viti maalumu kutoka mkoani Singida Martha Mlata”  alisema Sanga.



Alisema katika tamasha hilo kutakuwa na waimbaji zaidi ya 20 ambao  watatoa burudani baadhi yao ni muimbaji nguri Rose Mhando, Upendo Nkone, Emanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ Edson Mwasabwite, Stellah Joel na wengine wengi na kuwa kiingilio kitakuwa ni sh.5,000 kwa viti vya kawaida na sh.10,000 kwa viti maalumu.



Sanga alisema kauli mbiu ya tamasha hilo na uzinduzi wa albamu hiyo ni Amani na Utulivu vilivyopo nchini vidumishwe daima na alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo muhimu la kuliombea taifa.


(Imeandaliwa na mtandao wa www,habari za jamii.com)

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles