Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Pale unapoweza kupambana na hofu ya kushindwa ndipo unapoweza kufanikiwa kufanya jambo fulani katika maisha yako. Hapa tunakupa baadhi ya vitu vya kufanya kupamban na hofu.
Unatakiwa kujua kuna wakati mwingine maishani utashindwa. Kitu ambacho unatakiwa kufahamu kwenye maisha kwamba wewe ni binadamu na hufanya makosa. Kabla ya kuanza kutembea ili kubidi utambae, uanze kujifunza kusimama hatimaye kutembea. Katika hatua zote hizo ulishindwa wakati mwingine lakini uliinuka na kuendelea kujifunza mpaka ukaweza.
Unaposhindwa usichukulie jambo kibinafsi. Angalia wapi umeshindwa na ikusaidie kwenda hatua nyingine. Unaposhindwa jifunze kwanini umeshindwa na kujifunza kutokana na makosa yako. Usiishie tu kushindwa au kukubali kuwa umeshindwa au ni udhaifu ulionao, hapanaukiwa na mawazo hayo hautaweza kufikia mafanikio yako.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kumbuka kushindwa kwingi kumeleta mafanikio mengi duniani. Hebu fikiri katika historia watu wengi walivyojaribu mambo na wakashindwa kama wakina Newton, Einstein na wengine lakini hawakukata tamaa na wakafanikisha walichokuwa wanataka hivyo kusaidia maendeleo makubwa sana ya teknolojia ya leo.
Unatakiwa Ujiamini. Unapokata tamaa haikusaidii bali unahitaji kujenga uvumilivu na kurekebisha pale panapohitajika.Unatakiwa kuamini kwamba utafanya juhudi na kufanikisha hila jambo hata utakapopitia hatua au nyakati ngumu. Unatakiwa kujikumbusha kuwa watu wangapi walishindwa na kwasababu hawakukata tama wakafanikiasha walichokitaka? Wewe sio mtu wa kushindwa hata kidogo ukiamua kufanya jambo