Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Uongozi wa Skylight Band unawaomba radhi mashabiki wake wa Dar es Salaam kwa kutokuwepo nchini kwa ajili ya kutoa burudani jioni ya leo kwenye uwanja wao wa nyumbani Thai Village Masaki pamoja na siku ya Jumapili kwenye Skylight Sunday Bonanza katika kiota cha maraha Escape One kutokana na kupata mwaliko wa kutumbuiza nchini Oman.
Skylight Band watarejea nyumbani wiki ijayo na kuendelea na ratiba zao kama kawaida ambapo siku ya Ijumaa tarehe 10/10/2014 watakuwepo Thai Village pamoja na Jumapili tarehe 12/10/2014 kwenye Skylight Sunday Bonanza ndani ya kiota cha maraha Escape One.
Skylight Band inarudia tena kuwaomba radhi mashabiki wake wa Dar na kuendelea kuwashukuru kwa sapoti wanayoipata na inawapenda sana.