Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mratibu wa Tamasha, Ibrahim Sanga. |
Dotto Mwaibale
WAIMBAJI wa Nyimbo za Injili nchini wanatarajia kufanya tamasha kubwa la kuombea Taifa amani hasa katika kipindi hiki cha mchakato wa Katiba Mpya unaoendelea mjini Dodoma.
Akizungumza na mtandao wa www.habari za jamii.com Dar es Salaam leo mratibu wa tamasha hilo ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za injili, Ibrahim Sanga alisema ni muhimu kuliombea taifa wakati huu kutokana na umuhimu wake.
Sanga alisema tamasha hilo litakalokwenda sanjari na uzinduzi wa albamu ya Mungu ni Mwema litafanyika oktoba 12 mwaka
huu Hoteli ya Land Mark Ubungo.
"Tumejipanga vizuri kwa tamasha hilo ambalo litahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na dini na mgeni rasmi atakuwa ni Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenister Mhagama ni miongoni mwa wageni waalikwa watakao kuwepo" alisema Sanga.
Alisema katika tamasha hilo kutakuwa na waimbaji zaidi ya 20 ambao watatoa burudani baadhi yao ni muimbaji nguri Rose Mhando, Upendo Nkone, Emanuel Mgaya 'Masanja Mkandamizaji' Edson Mwasabwite, Stellah Joel na wengine wengi na kuwa kiingilio kitakuwa ni sh.5,000 kwa viti vya kawaida na sh.10,000 kwa viti maalumu.
Sanga alisema kauli mbiu ya tamasha hilo na uzinduzi wa albamu hiyo ni Amani na Utulivu vilivyopo nchini vidumishwe daima na alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo muhimu la kuliombea taifa.