Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Siku hizi ni kawaida kwa mtu kukubali kazi ambayo hata hajasomea kwa sababu kazi zimekuwa ni za shida sana. Kukosa kazi na ongezeko la ushindani na urasimu katika kutafuta kazi hata haukusaidii, kwani unahitaji kulipa bili za maji, umeme na kujikimu kwa mahitaji mbalimbali, hivyo kazi lazima ipatikane.
Vile vile ni vigumu kuwa na furaha katika kazi ambayo hujaipenda ila kwasababu inakusaidia kuishi mjini inabidi uendelee kuifanya. Je unaboresha vipi ujuzi wako kwa ajili ya kazi inayofuata?
Kama una wasiwasi hutapata uzoefu unaohitaji, kuna vitu vitatu ambayo unaweza kuvifanya kujiimarisha kitaaluma;
1. Kwa juhudi kubwa tafuta namna ambayo unaweza kutumia ujuzi wake hapo ulipo.
Inawezekana wewe in mwandishi ila unafanya kazi za mauzo na utafutaji wa masoko, kama unafanya kitu ambacho hujasomea na fani yako ipo kapuni jaribu kutafuta namna ambavyo unaweza kuitumia hapo hapo ulipo.
Kwa mfano kama wewe ni mwandishi ila unafanya kazi nyingi zinazohusu uongozi ili taaluma yako isipotee anza kuandika kwaajili ya mashirika ya habari hiyo itaboresha taaluma yako na kukupeleka viwango vingine. Unaweza kusaidia katika tuvuti ya kampuni hiyo kuandika makala mbalimbali na kuifanya ionekane tofauti kwenye mitandao ya kijamii. Hii inawezekana kwa mtu ambaye anataka taaluma yake isipotee na si vinginevyo.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
2. Omba bosi wako akuongezee majukumu
Hilo ni jambo gumu kulifanya na kila mtu anatamani kupunguza majukumu. Kitu ambacho unatakiwa kujua kama unataka kuipa changamoto taaluma yako ni kufanya vitu vigumu vinavyohusu taaluma hiyo. Na kitu kinakufanya uonekane wa tofauti kwa mwajiri wako ni kumwonyesha bosi wako kuwa huogopi changamoto kwa kuwa ni wachache wanaoweza kufanya hivyo. Hizi ni zama za ushindani mkubwa inabidi taaluma yako ing’ae sana.
3. Anzisha blog yako na kutumia vizuri mitandao ya kijamii
Unapoanzisha blogu yako jifunze namna ya kutangaza biashara yako na taaluma yako kupitia namna ambavyo unaandika makala mbalimbali. Kufanya Mambo ya namna hii kutafanya watu waendelee kukutafuta na vile vile unaweza ukapata mwajiri mwingine ambaye atataka umfanyie kazi zake kulingana na ushauri unaotoa katika kila unachokiandika.
Jinsi unavyoifahamu biashara ya mwajiri wako ndivyo kazi yako inaendelea kuwa rahisi. Ukiacha kujifunza leo hutoweza kufanya kitu kipya kesho.