Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mtoto, Daniel Julius Mushi (12), mlemavu asiyetembeaanayetunzwa ndani kwa miaka 9 bila kutoka nje tangu 2005. (Picha na Bryceson Mathias)
Kushoto na Kulia ni Julius Mushin na Mkewe Ester Kwayu, Wazazi wa Mtoto, Daniel Julius Mushi (12), wa Katikati, ambaye ni mlemavu anayetunzwa ndani kwa miaka 9 bila kutoka nje tangu 2005.
Na Bryceson Mathias, Kikuyu Dodoma
MTOTO Mlemavu, Daniel Julius Mushi (12) pichani, wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Iringa Road, Jumuia ya Mtaa wa Kikuyu Dodoma, amekuwa akikaa ndani ya nyumba ya Wazazi wake kwa miaka Tisa (9) sasa!.
Wakizungumzia hali hiyo Nyumbani kwao hivi karinuni Wazazi wake, Julius Mushi na Ester Kwayu, walisema hawana njia ya kumfanya mtoto huyo atoke hapo alipo, isipokuwa kwa kuomba Msaada wa Mungu na Ushauri wa Mawazo ya Wasamalia wema wawasaidie.
“Baada ya Mtoto wetu kuzaliwa alilemaa, pamoja na jitihada tulizofanya kwa miaka mitatu; hatukufanikiwa ameendelea kukaa ndani bila kwenda kokote miaka Tisa (9) sasa, hivyo tunamuomba Mungu atuinulie watu wampe Vifaa Tiba vimsaidie hata atoke nje na kurudi ndani.
“Nikiwa na Shughuli namuacha ndani amelala au amekaa kwenye Kochi ‘kama alivyo hapo’ pichani, sana atajigeuzageuza tu, ndiyo maana tunaona afadhali alale ndani kwa kuwa kwenye Kochi anaanguka, hivyo tunaomba msaada”.alisema Mama Kwayu kwa Uchungu!.
Mtoto huyo Hasemi vizuri, Hatembei, isipokuwa Kukaa, Kucheka, akitoa Mate mdomoni; Miguu na Mikono yake imelemaa tangu akiwa na umri mdogo, ambapo Mama yake Kwayu, alisema, hali hiyo ilimuanza kwa kuwashwa puani, na alipojikuna, hali hiyo ilitokea.
Wazazi hao wamewaomba Watalaam na Waumini wa dini zote wenye Mapenzi Mema, wawasaidie ili mtoto wao apate Vifaa Tiba vitakavyomsaidia kutoka nje na kurudi ndani, ikibidi aweze kusoma Shule za Walemavu walio kama yeye, ili aepukane kutunzwa na kukaa ndani.
Walipoulizwa namba zao za simu iwapo Wasamalia wema ama Watalaam na Walimu wa watoto hao watataka kutoa mawazo au msaada wowote wa vifaa tiba, Shule au Matibabu, Baba wa Mtoto huyo alisema; “Watushauri kwa Namba 0755-091656, Mke wangu ni 0754-826419”.
Mmoja wa Majirani aliyeomba asitajwe alisema, watoto waliozaliwa naye akiwemo mwanae, wako Darasa la Sita, na mwaka huu wataingia darasa la Saba, lakini yeye bado anaendelea kuteseka kwa Masahibu hayo huku wazazi wakimsaidia hata kumlisha na Maliwato.