Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mshindi wa taji la Redd’s Miss Tanzania Top Model 2014, Jihan Dimachk (katikati) akipozi kwa picha na mshindi wa pili Doreen Robert (wapili kulia), mshindi wa tatu Evelyn Baasa ambaye pia ni Miss Tanzania Photogenic 2014 (wapili kushoto), mshindi wa nne, Lilian Timothy (kulia) na Mshindo wa tano Nasreen Abdul, mara baada ya kushinda taji hilo jana ambapo Jihan amekuwa mrembo wa pili kuingia katika nusu fainali za Miss Tanania 2014 baada ya Miss Photogenic. Shindano la Miss Tanzania Top Mode lilifanyika katika ukumbi wa Triple A jijini Arusha na kuwashirikisha warembo 30..Picha/Father Kidevu Blog
Warembo wakipita jukwaani wakiwa wamevalia nguo za mbunifu Zakia Disign wakati wa shindano hilo.
Washiriki wakipita jukwaani na mavazi maridhawa kutoka Trecy Fashion ya jijini Arusha.
Jopo la majaji wakiwa katika meza yao tayari kwa kutoa hukumu kwa walicho kiona. Wadau wa urembo kutoka, Chuo cha Chuo Kikuu Iringa (Tumaini) na Makumira jijini Arusha wakifuatilia shindano hilo ambapo mwenzao Martha John alikuwa akitupa karata yake jukwaani.
Mwana dada Vanesa Mdee na kikosi kazi chake walishambulia jukwaa vilivyo wakati wakisindikiza shindano hilo usiku huu.Wadau mbalimbali wa sanaa ya urembo na mitindo jijini Arusha wakiwa wamejumuika katika shindanohilo.
Mbunifu wa mavazi, Zakia akipozi kwa picha.
Mtangazaji wa kipindi cha burudani cha Funika Base kutoka Radio 5 ya Mjini Arusha , Julius Kamafa ndiye alikuwa mshereheshaji katika shindano hilo.
Mwanasheria Machachari wa Jijini Arusha, Albert Msendo (kulia) akiwa na mkali wa Bongo Fleva, Mwana FA wakifuatilia shindano hilo.