Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

BAWACHA WATOA KAULI YA KUIPIGA KATIBA MPYA

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 

Mwenyekiti wa BAWACHA, Mh. Halima Mdee  akizungumza na wanahabari jijini  Dar es salaam(hawapo pichani).
            Baraza la wanawake wa chama cha democrasia na maendeleo chadema (BAWACHA) wamekuwa wa kwanza kuipinga rasimu ya tatu iliyowasilishwa bungeni jana na kutangaza kuandamana hadi ikulu ya jiji la dar es salaam kupeleka kilio chao kwa kile walichoitwa kushindwa kuwapa wanawake nafasi stahiki katika rasimu hiyo.

           Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwenyekiti wa BAWACHA ambaye pia ni mbunge wa Kawe, Mh. Halima Mdee amesema kuwa kuwapa wanawake nafasi za uongozi za hamsini kwa hamsini kama rasimu hiyo ilivyoelekeza bado sio kipaumbele cha wanawake wa Tanzania ila kinachofanyika ni kuendelea kuwalaghai wanawake wa Tanzania.


ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBFYA HAPA CHINI

            Aidha amesema kuwa rasimu hiyo bado haimjali mtanzania kwani kuna mambo mengi ambayo yameondolewa yalikuwepo kwenye rasimu ya Jaji Warioba.

            Wanawake hao wametangaza kufanya maandamano wiki moja ijayo ambayo amekataa kutaja siku rasmi kwa kile alichokisema kuwa bado wanafanya maandalizi ambapo yatakuwa  ya amani ambapo amewataka polisi kuwalinda kwani maandamano hayo yatakuwa ya amani na utulivu mkubwa yakiwa na lengo la kupeleka ujumbe kwa watanzania wote juu ya mchakato huo wa katiba.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>