Watu wawili wamefariki dunia baada ya ajali iliyolihusisha gari aina ya Mitsubishi Canter lililosajiliwa kwa namba T. 497 AFR lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Sefania Msigalamwenye miaka 40 ambaye ni mkazi wa Madabaga mkoani hapa.
Taarifa kutoka kwa maafisa wa polisi mkoani Mbeya zinaeleza kuwa ajali hiyo imetokea baada ya gari hilo kuacha njia na kupinduka alfajiri ya kuamkia leo majira ya saa 10:15 katika mteremko mkali kijijini Itewe, wilaya ya Mbeya vijijini mkoani hapa na kisha kusababisha kifo
cha Dereva wa gari hilo Sefania Msigala na abiria wake Riziki Mhanga mwenye miaka 45 mkazi wa Njombe.
cha Dereva wa gari hilo Sefania Msigala na abiria wake Riziki Mhanga mwenye miaka 45 mkazi wa Njombe.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika ingawa bado kinachunguzwa huku miili ya marehemu ikihifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.