1.Tegemea kukutana na kipindi kigumu cha kukosa fedha, wazazi hawatakuwa karibu na wewe sana kama ulipokua mdogo. Jiandae kujifunza kupambana na kutimiza baadhi ya mahitaji yako.
2. Utaangukia pua mara kadhaa pengine kutokana na kazi, mapenzi, elimu nk. Cha Muhimu ni kuamka haraka iwezekanavyo na kujifunza kutokana na makosa.
3.Usitegemee kuishi eneo moja (pengine ulilozaliwa) Tegemea Kutengana na marafiki zako wengi wa zamani pengine kutokana na kubadili eneo la makazi, shule, kazi nk vitakavyokuchukulia muda wako mwingi na utapata marafiki wapya (isikupe shida)4.Katika muda huu, utakuwa na vitu vichache sana vya kudumu kuanzia makazi, marafiki au hata kazi. Jiandae kwa hayo kwani ushakuwa mtu mzima.
5.Utakutana na Watu wengi zaidi wanaopingana na wewe. Pengine itakufanya usijiamini tena lakini ndio hali halisi, ikabili! kwani ukishindwa, huu ndio mwanzo wa kuyaogopa maisha na kuwa masikini.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
6. Kwa mara ya kwanza tegemea kukutana na ugumu wa maisha (uso kwa uso). Kile ulichukuwa ukikisikia kinaitwa “Changamoto” sasa kiko mlangoni japo changamoto hizo hazitakuja kwa haraka au kwa wakati mmoja.
7. Wazazi au ndugu zako wa karibu watakuacha ufanye baadhi ya mambo mwenyewe, ule ukaribu wao kwako utapungua na kuna wakati utajihisi mpweke sana lakini sasa unahitaji ubadili namna yako ya kawaida ya kufikiria.