Mabaki ya miili ya watu ambao baadhi ya vyanzo vinasema ni zaidi ya 100 imekutwa katika msitu mdogo uliopo eneo la Mpiji, kata ya Mbweni, wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, ikiwa imetelekezwa.
Mabaki hayo ya miili yalionekana jana katika eneo hilo majira ya jioni na kuvuta mamia ya wananchi waliokwenda kushuhudia tukio hilo. Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema , mabaki yalikuwa yamehifadhiwa katika mifuko ya plastiki ikiwa imefungwa juu.
Alisema mabaki hayo ambayo yamekaushwa na kuhifadhiwa katika mifuko ya ujazo wa kilo 25 ni pamoja na miguu, mikono, mbavu na mafuvu ya vichwa.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Alisema waliobaini kuwapo kwa mabaki hayo ni majirani wa eneo hilo ambao walitoa taarifa polisi.
Polisi walifika eneo la tukio na kuanza kupakia mabaki hayo katika gari lao lenye namba za usajili MS 54 UKH na kuipeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alipoulizwa alisema wakati huo alikuwa eneo la tukio na kwamba angetoa taarifa baadaye.
Chanzo: EATV