Mchezaji wa timu ya Brazil, Neymar hatoendelea na michuano ya Kombe la Dunia 2014 baada ya kuvunjika mfupa unaoshikana na uti wa mgongo wakati wa mechi yao na Colombia usiku wa kuamkia leo.
Neymar akilia kwa uchungu baada ya kuvunjika mfupa.
Staa huyo mwenye mabao manne mpaka sasa kwenye michuano hiyo, alitolewa uwanjani dakika tatu kabla ya mechi yao dhidi ya Colombia kumalizika.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Neymar akiwa chini baada ya kuvunjika mfupa.
Katika mechi hiyo, Brazil walishinda mabao 2-1 na kutinga Nusu Fainali ambapo watakutana na Ujerumani Julai 8 mwaka huu. Neymar akipatiwa huduma ya kwanza.
Kwa mujibu wa taarifa za daktari wa timu ya Brazil, Neymar atakaa nje kwa takribani wiki nne.
Wapenzi wa soka nchini Brazil wakiwa nje ya hospitali aliyopelekwa Neymar.