Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

SHAKIRA, WYCLEIF JEAN NA CARLOS SANTANA KUTUMBUIZA KWENYE FAINALI YA KOMBE LA DUNIA

$
0
0
Muimbaji mrembo mwenye asili ya Colombia, Shakira atatumbuiza kabla ya mechi ya fainali ya kombe la dunia itakayofanyika Rio de Janeiro,Brazil, July 13.
Wengine watakaotumbuiza siku hiyo ni mcheza gitaa maarufu Carlos Santana na rapper Wyclef Jean. Shirikisho la soka duniani, FIFA limesema Shakira, ambaye atatumbuiza kwa mara ya tatu mfululizo kwenye fainali za kombe la dunia ataimba wimbo La la la (Brazil 2014) na muimbaji wa Brazil, Carlinhos Brown.
Santana, Wyclef na muimbaji wa Brazil, Alexandre Pires watatumbuiza wimbo rasmi wa mashindano hayo, “Dar Um Jeito” kwenye uwanja Maracana.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>