Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

ZITAMBUE NDOTO 10 ZINAZOOTWA ZAIDI USIKU NA MAANA ZAKE

$
0
0
Ndoto ni jambo au hisia ya kawaida inayompata mtu alalapo usiku. Kwa mujibu wa gazeti la The Mirror la Uingereza, hizi ni ndoto 10 zinazootwa zaidi na maana yake.

1. Kuota watu: Watu katika ndoto yako wanaweza kuwakilishia sifa za wajihi wako mwenyewe ambao unatakiwa kufanyiwa kazi.

2.Kuota mwili umekosa nguvu/kama umepooza: Katika ndoto hii ni kweli mtu hujisikia kama mwili umepooza wakati akiota na hiyo humaanisha kuwa mtu huyo amepoteza control katika maisha yake.


ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


3.Kuota unaanguka: Hii inaweza kumaanisha kuwa mambo katika maisha yako hayaendi vizuri. Inaweza kuwa kazini, uhusiano au masuala ya fedha.

4.Meno: Kuota umetoka meno kunamaanisha kuwa una uoga wa kujiona hauna mvuto na inaweza kuhusiana na hisia ya kujiona umefedheheshwa na kitu maisha mwako.

5. Kuota Unakimbizwa: Utakuwa unaepuka hisia inayokutisha ama ikuumizayo, mtu ama jambo fulani baya.

6.Kifo au Ugonjwa: Uko mbioni kuugua ama inaweza kumaanisha kuwa hauumwi kimwili bali kimawazo au unaogopa kuumizwa.

7. Kuwa mtupu: Kuota ukiwa utupu hadharani inamaanisha kuwa hisia za udhaifu ama kugundulika. Hisia hizo zinaweza kupishana kuanzia aibu au kujisikia upo huru au sifa.

8.Kuota Maji: Kunamaanisha mabadiliko au vitu vipya. Inaweza kumaanisha pia kuhusu kubadilika mambo/vitu katika maisha yako.

9. Kuota vyombo vya usafiri: Ndoto hizi huonesha muelekeo ambao maisha yanatupeleka.

10. Kuota umeshikwa/umepotea: Ndoto hii hutokea pale unapokumbuna na ugumu katika kuchukua uamuzi kutokana na jambo lililo mbele yako.



NA BONGO 5

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>