Viongozi wa Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise, wakipanda mti wakati wa Uzinduzi wa Kampuni hiyo iliyoambatana na utoaji wa Msaada wa Vifaa vya Michezo na vya mafunzo ya kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na kutunza mazingra katika Shule ya Sekondari Miono na Kikaro zilizopo Chalinze Mkoa wa Pwani.
Mbia wa Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise, inayotoa elimu ya kupambana na mazingira madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo Mashuleni, Said Said kulia akimkabidhi msaada wa vifaa vya kuelimisha wanafunzi jinsi ya kuepukana na matumizi ya madawa ya kurevya Mwalimu wa Shule ya Sekondari Miono, Ally Miango shuleni hapo juzi.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mbia wa Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise, inayotoa elimu ya kupambana na mazingira madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo Mashuleni, Adam Kasale, kushoto akimkabidhi msaada wa vifaa vya michezo Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kikaro, Gabriel Dominc baada ya Kampuni hiyo kutoa msaada kwa shule hiyo na Miono zilizopo Chalinze Mkoa wa Pwani, katikati ni Mkuu wa Mkoa huo, Mwamtum Mahiza.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kevin William na Alex Mode wa Shule ya Kikaro wakichuana kuwania mpira baada ya kupokea msaada wa Vifaa vya Michezo na vya mafunzo ya kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya uliotolewa na Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwamtumu Mahiza kulia akimkabidhi Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kikaro, Alex Mode, mbuzi aliyetolewa na Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise inayotoa elimu ya kupambana na mazingira madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo pia kampuni hiyo imetoa vifaa mbalimbali vya michezo katika shule mbili hizo. Miono Kikaro zilizopo Chalinze Mkoa wa Pwani.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari, Kikaro wakiwa wamembeba juu juu mbuzi waliopewa na Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise, inayotoa elimu ya kupambana na mazingira madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo baada ya kuifunga timu ya Shule ya Sekondari Miono kampuni hiyo pia imetoa vifaa mbalimbali vya michezo katika shule mbili hizo.