Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

ZIFAHAMU TABIA SABA(7) ZA WATU AMBAO HUPANDISHWA VYEO

$
0
0

  
Kama una ota ndoto ya kuwa kwenye ofisi nzuri huku watu muhimu wakisubiri kusikia simu yako, au umechoka kuwa mtu wa kawaida ofisini ambaye hutambuliki kwa lolote lile na sasa unataka kutambulika, hii inakuhusu.Kila kitu unachofanya ili upandishwe cheo, kuna baadhi ya vitu ambavyo unatakiwa kuvijua. Kwa wanaofanya kazi serikalini inaweza kuwa ngumu sijui wao huwa wanafanyaje, kwa taasisi binafsi hizi zinaweza kukufikisha mahali fulani. 

1. Kujitoa kwa hali na mali 
Uvumilivu na kusimamia kufanya kile unachokiamini na tabia za watu ambao hufikia malengo na nyazifa za juu katika biashara na makampuni mbalimbali yaliyofanikiwa. Hakuna taaluma iliyo sahihi na hakuja mradi ambao hautakosewa kwa kiasi fulani kitu kinachojalisha ni kwamba umewezaji kuinuka baada ya makosa au kushindwa? 

2. Jenga Urafiki na Watu wengine 
Watu waliofanikiwa ni wale ambao hawajali dana dana watu wanaowazunguka au maisha ya kijamii kama michezo ,kujumuika pamoja na watu wengine . Wao hufanya kazi kwa bidii nyingi na kuangalia sana mafanikio yao bila kuhusiana na watu wengine. Watu wanofanya hivyo waliofanikiwa ni wachache sisi wengine tunahitaji kuhusiana na watu wengine kwanza inakuongezea kufahamika na mile unachofanya kufahamika pia. Hivyo usifanye makosa ya kudharau matukio yanayohusianisha wafanyabiashara wa like yako au wafanyakazi wenzako wa like yako. Jenga urafiki na watu wengine na kuhusiana nao na update fursa kutokana na urafiki huo.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KW KUBOFYA HAPA CHINI
3. Ujasiri
Ujasiri ni kitu kingine. Unaweza kuwa jasiri kwenye vikao lakini ukawa mzembe kwenye mambo ya kuchangamkia fursa. Ujasiri tunaouzungumzia ni uwezo wa kuchukua hatua ya kuanzisha kitu bila yoga wala wasiwasi, uwezo wa kuzikabili changamoto na kushinda au ukishView blogindwa una ujasiri wa kuinuka tena. Je ni kitu gani kinakufanya ufanye maamuzi fulani na ukaamua kusonga mbele na maaamuzi hayo?

4. Uwezo wa kuweka kipaumbele
Kama jambo ni la muhimu lakini si la kupewa kipaumbele cha kwanza huwa unafanya nini? Ili uweze kufanikiwa na kupewa nafasi za juu, unatakiwa uwe mtu wa kujua je jambo hili ninatakiwa kulipa kipaumbele au la!

5. Je unajiwajibisha?
kama unataka kufanikiwa unatakiwa kuwajibika katika kila unachofanya, hata kama hicho au mambo hilo sio la kwako moja kwa moja! Inawezekana bosi wako hawezi kuyaona makosa yanapotokea kwenye kitengo chenu. Je wewe unawajibika vipi kumsaidia kama kosa hajaligundua na wewe umegundua? Mwingine atafikiri ni kujipendekeza, ndio maanza nimezungumzia taasisi zilizokua na sio serikalini, tunazungumzia scheme ambazo unaweza kukua kitaaluma na ukaleta tina ya hali ya juu.
Inawezeka unafanya kazi na watu wenye masiala mengi ambao wanasubiri tu mshahara au dili ndipo waonyeshe kwamba wao wanahusika kufanya kazi fulani. Ninazungumzia watu wenye uelewa wa kufanya kazi na ambao wanamalengo ya kukuza taaluma zao. Je wewe unawajibika? 

6. Je unachukua hatua za kuanzisha jambo?
Hakuna mtu anaweza akakupa kazi nzuri hata kama unastahili, unahitaji kuanzisha kitu kwa nguvu. Kitu cha kuanza nacho ni hayo majukumu uliyonayo na kuyafanya sambamba na fursa ya kufanya kitu kipya na ukifanyie kazi. Kama siku zote ofisini watu wanalalamika kuhusu network za mafaili yenu hapo kazini ni mbaya fikiria njia mbadala ambayo italeta tija na sio kukaa na kulalamika kila siku. Hivyo tengeneza bajeti ya mbadala huo na sababu yake halafu wasilisha kwa bosi wako.

7. Utayari wa Kubadilika
Je uko tayari kubadilika , kujifunza vitu vipya na kuboresha utendaji wake? Je unaongeza ujuzi wake katika taaluma yako? Kama unafikiria tu kuhusu kupandishwa cheo wakati wewe mwenyewe huonekani kama ni mtu anayeweza kupandishwa cheo, unapoteza muda wako. Kupandishwa cheo sio mara zote ukiongeza shahada ya pili, utendaji wako ukoje na umeongeza ujuzi gani katika utendaji wako? Unaweza kuwa na cheti kizuri lakini huwezi kufanya kazi inavyopaswa hivyo usishangae kwanini hupandishwi cheo.

Na  Bongo 5

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>