Mariam Osher Mmarekani mchoraji aliyetembelea mbuga za wanyama Tanzania na kubuni uchoraji wa wanyama aliowaona huko Tanzania na kutumia michoro hiyo kuitangaza Tanzania kwa Wamarekani na raia wengine ambao wajawahifika Tanzania kwenye maonesho ya picha zake yaliyofanyika leo Silver Spring, Maryland kwenye ukumbi wa WPG uliopo 8230 Georgia Ave.
Mhe. Liberata Mulamula , Balozi wa Tanzania nchini Marekani (wapili toka kulia) akiwa pamoja na Afisa wa Ubalozi kitengo cha Utalii Bi. Immaculata Diyamett wakifuatilia maelezo ya Marian Osher.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Balozi Liberata Mulamula pamoja na Afisa Immaculata Diyamett wakifuatilia maelezo ya Marian Osher
Juu na chini ni watu mbalimbali waliofika kwenye onesho hilo la Marian Osher.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akitoa shukurani zake kwa Marian Osher huku akiongea na watu waliofika kwenye onesho hilo kuwaelezea vivutio vilivyopo kwenye mbuga zetu za wanyama.