Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

PADRI WA KANISA KATOLIKI NA KATEKISTA WAFA AJALINI WAKATI WA MAPOKEZI YA ASKOFU NYAISONGA

$
0
0
Askofu Gervas Nyaisonga wa Jimbo katoliki la Mpanda akibusu Ardhi hapo jana katika kijiji cha Kamsisi ikiwa ni ishara ya kuhamia rasmi kuliongoza jimbo la Mpanda akitokea jimbo katoliki la Dodoma
Askofu Gervas Nyaisonga wa jimbo la Katoliki la Mpanda akisalimiana na Mapadri wa jimbo hilo katika eneo la mto koga Hapo jana ambapo ndipo linapoanzia Jimbo katoliki la Mpanda wakati alipokuwa akiwasili rasmi kwenye jimbo lake jipya la Mpanda akiwa anatokea jimbo la Dodoma.

ENDELEA KUSOMA HABARI HIII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Askari wa skauti wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda wakiwa katika eneo la daraja la mto koga wakimpokea askofu Gervas Nyaisonga alipowasili hapo jana akitokea jimbo la Dodoma ambapo askofu Nyaisonga alipokuwa analiongoza kabla ya kuhamishiwa Jimbo la Mpanda na amesimikwa jana kuwa askofu wa Jimbo la Mpanda
Msafara wa waendesha pikipiki wakiwa katika eneo la uwanja wa ndege mjini Mpanda wakiwa wanaongoza msafara wa kumpokea askofu Gervas Nyaisonga hapo jana ambae amehamishiwa jimbo la Mpanda akitokea jimbo la dodoma
Mapadri wa kanisa katoliki wakiwa kwenye kanisa kuu la jimbo Katoliki la Mpanda kabla ya kuanza kwa ibada ya kukabidhiwa ufunguo wa kanisa hilo askofu Gervas Nyaisonga ambae amehamishiwa jimbo la Mpanda ikiwa ni ishara ya kuyaongoza makanisa na kuyasimamia makanisa yote ya jimbo katoliki la Mpanda 
Picha na Walter Nguluchuma 

Na Walter Mguluchuma

Padri wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Mpanda Padri Matini Kapufi (42 ) pamoja na Katekista wa Kanisa hilo wa KijiJI cha mtakuja Parokia ya Inyonga Katekista Patricki Mwendo wa Saa (60) wamefariki Dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka baada ya gari kuacha njia na watu wengine wawili kujeruhiw na kulazwa hospitalini

Kwa mujibu wa Kamanda wa jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari ajari hiyo ilitokea hapo juzi majira ya saa nne asubuhi katika Kijiji cha Kamsisi tarafa ya Inyonga barabara ya Inyonga kuelekea Mkoani Tabora

Alisema ajari hiyo ililihusisha gari aina ya Toyota Hilux pick Up lenye namba za usajiri T 302 CUY lililokuwa likiendeshwa na Marehemu Padri Martini Kapufi ambae ni Paroko wa parokia ya Mwese jimbo katoliki la Mpanda
Kidavashari aliwataja watu waliojeruhiwa kwenye ajari hiyo kuwa ni Daud Saveli (31) katekista msaidizi wa kijiji cha Mtakuja parokia ya Inyonga, ambae ameumia sehemu ya kidevu chake na mguu wa kushoto na melikio Maraluma mkazi wa kiji cha mtakuja Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mlele

Alisema watu hao walipata ajari wakati wakiwa wanasafiri kutoka Inyonga makao makuu ya Wilaya ya mlele wakiwa wanaelekea eneo la Mto Koga mpakani mwa Mkoa wa Katavi na Tabora kwa lengo la kwenda kumpokea Askofo Gervas Nyaisonga aliyekuwa akitokea Dodoma ambae ameamishiwa jimbo la Mpanda akitokea jimbo katoliki la Dodoma

Kamanda Kidavashari alieleza kuwa watu hao ndipo walipokuwa wakisafiri na gari hiyo na walipofika katika maeneo ya kijiji cha Kamsisi gari hiyo iliacha njia na kupinduka ambapo Katikista Patrick Mwendowasaa alifariki hapo hapo mara baada ya kutokea kwa ajari na Padri Martini Kapufi alifariki njiani wakati akiwa anapelekwa kwenye kituo cha afya cha Inyonga

Alisema majeruhi wote wawili wamelazwa katika kituo cha afya cha Inyonga wakiwa wanaendelea kupatiwa matibu huku hali zao zikiwa zinaendelea vizuri na miili ya marehamu hao wawili imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha kituo cha afya cha Inyonga

Kamanda Kidavashari alieleza kitengo cha jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kinaendelea na uchunguzi ili kuweza kubaini chanzo kilichosababisha ajari hiyo ya gari mali ya jimbo Katoloki la Mpanda.:

Chanzo: Katavi yetu Blog

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>