Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

KAMA UNATAKA MABADILIKO LAZIMA YAANZE KWAKO MWENYEWE

$
0
0
Tunaongelea mabadiliko mara nyingi katika nyanja mbalimbali, na tumekuwa tukipiga kelele ya mabadiliko kila sehemu na kuleta maneno mengi ya busara na hekima kwanini tunahitaji mabadiliko. Je sisi si watu wakushangaza? au sisi ni wanafiki tu?

Thamani ya Mabadiliko:
Watu wengi waliosoma au wenye elimu hupenda kutamka mabadiliko lakini huwa ngumu pale ambapo huyo anayeongea anatakiwa kubadilika. Hili siliongelei kwa kuongea jukwaani tu bali katika maisha ya kila siku hata mimi mwenyewe utata huanza. Nilikuwa nikifanya kazi kwenye kampuni moja hapo kabla ambalo limefanikiwa sana miaka ya nyuma na kila wakati tulikuwa tunasikia wakubwa wengi wakisema mabadiliko yaweko kwa namna tunavyotafuta masoko na tunavyofanya biashara. Kila mtu alifurahia kauli hizo za mabadiliko na kuwa na hamu ya kuona mabadiliko yanatokea.
Mabosi wa kampuni hiyo walihitaji sana mabadiliko yatokee kwenye masoko, watu wa mauzo na kampuni kwa ujumla katika suala la utendaji. Kazi ilianza kuwa ngumu pale ambapo wafanyakazi wote wako tayari kupokea hapo mabadiliko kumbe tatizo liko kwao wenyewe kwani wanahitaji kubadilika namna wanavyoendesha hiyo kampuni. Hawakuweza kufanya mabadiliko kwakuwa tatizo lilikuwa kwao wenyewe na kuiacha kampuni ikifa bila msaada wowote.

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Suala huwa gumu pale ambapo mtu anayehitaji mabadiliko yatokee yeye ndiye anatakiwa kubadirika, chuki na hasira hutawala maamuzi hayo magumu au mabadiliko kutotokea kabisa. Kama unataka mabadiliko yatokee unahitaji kuchukua hatua binafsi wewe kama wewe. 

Mabadiliko huanza na wewe mwenyewe!
Hiki ndicho nimejifunza kwamba ukitaka mabadiliko wewe unatakiwa uwe wa kwanza kubadilika. Huwezi ukawaambia watu waongeze juhudi wakati wewe huonyeshi juhudi hata kidogo, kama biashara yako inatakiwa kutoa bidhaa tofauti au huduma kwa namna ya tofauti mabadiliko lazima yaanze kwako mwenyewe unayetaka mabadiliko. Kuna usemi mmoja maarufu, husema hivi;
“Kila mtu anafikiria kubadilisha dunia lakini hakuna anayefikilia yeye mwenyewe kubadilika”
– Leo Tolstoy
kauli hiyo ni ya kweli kabisa, kama nataka kubadilisha mambo au maisha yanayonizunguka inanipasa nianze mwenyewe kubadilika ndipo ujumbe wa mabadiliko kwa watt winging utaleta maana. Biashara yako unawake ibadilike wewe unatakiwa ubadilike namna unavyoiendesha, badilisha mfumo wake kichwani ndipo ubadilishe mfumo mzima kwa watu wengine.
Gandhi yeye anasema:
“wewe mwenyewe uwe badiliko ambalo unawaza kuliona duniani ”
…ingawa ni ngumu, inapotokea kuna mabadiliko unawake yafanyike kwa wengine lakini sio kwako.

Badiliko Kubwa:
Badiliko kubwa litatokea kama tukibadilisha namna tunavyoyatizama mambo, namna tunavyohusiana na dunia inayotuzunguka. Ukweli ni kwamba ukibadilisha namna unavyoyatizama mambo na vitu ambavyo unataka vibadilike.
Ni kweli lakini kuna changamoto!
Wakati mwingine unahitaji mabadiliko angalia ndani yako kith gain unawake kibadilike. Anzia halo kwanza!

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>