Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi wa pili kutoka kulia pamoja na Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwasalimia akina mama Shujaa wa Chakula ambao wameingia Rasmi Kijiji cha Maisha Plus Jana usiku.
Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi wa katikati akitoa hotuba yake fupi wakati wa Sherehe za kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus, katika Hotuba hiyo aliwapongeza waandaaji na wabunifu wa Shindano hilo, pia Grow kupitia OXFAM kwa kuungana na Maisha Plus kuwaleta Mama Shujaa wa Chakula, Mwisho aliahidi kuongeza Milioni 5 kwa Mama Shujaa wa Chakula atakaye nyakua ushindi, Kutoa Milioni mbili na nusu kwa Mama Shujaa wa Chakula aliyepita ili zikamsaidie katika kilimo na Mwisho Kutoa Milioni Mbili kwa Washiriki wa Shindano la Maisha Plus ambao sasa wamebakia 16 mpaka mwisho wa Shindano Tarehe 18.05.2014
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Akina Mama Shujaa wa Chakula Wakiwa wanamuimbia wimbo maalum Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi mara baada ya kuwasili Kijijini hapo.
Hawa ndio Mama Shujaa wa Chakula ambao jana usiku wameingia Rasmi katika Kijiji Cha Maisha Plus
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhudia Kukaribishwa Rasmi kwa Mama shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus.
Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012 Sister Anna Mwasu wa tatu kutoka kulia akiwa katika sherehe za kuwakaribisha mama Shujaa wa Chakula ambao wameingia rasmi katika Kijiji cha Maisha Plus Jana.Mwakilishi kutoka Forum CC Faidhari akizungumza jambo wakati wa kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus.
Teresa Yates Mwakilishi kutoka OXFAM akitoa salama za Shukurani kwa wadau wote
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mh. Ahmed Kipozi akiwakaribisha Rasmi wageni wote katika Kijiji cha Maisha plus pia kumkaribisha Mgeni Rasmi Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi ili aweze kutoa hotuba yake
Mmoja wa washiriki wa Maisha Plus akisoma Jina la Mama yake ambaye atakuwa naye katika Kipindi hiki kilicho bakia cha Shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula.
Vijana na Washiriki wa Maisha Plus wakiwa na Mama zao walezi ambao ndio wameingia Rasmi kijijini Jana
Huyu Ndiye Mama Shujaa wa Kwanza kupata nafasi ya Kuwa Markia wa Kijiji cha Maisha Plus Mary J. Mwanga, na wa kwanza kulia ni Rais wa Kijiji cha Maisha Plus Abisai Caron kutoka kenya hapa akiwa anavishwa kofia ya utambulisho na Epheta Msiga Meneja Miradi kutoka DMB
Picha ya Pamoja Mgeni Rasmi Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi, Wakina Mama Shujaa wa Chakula, Vijana wa Maisha Plus pamoja na wadau mbalimbali waliofika katika sherehe za kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula Kijiji cha maisha Plus
Mkurugenzi Mtendaji wa DMB ambao ndio waendeshaji wa Shindano la Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula Ally Masoud(Masoud Kipanya) Akitoa utaratibu wa jinsi Akina mama Shujaa wa Chakula watakavyo ishi na vijana hao katika kijiji hicho
Mama Shujaa wa Chakula wakipata maelekezo Mbalimbali juu ya Kijiji Hicho
Moja ya Bendi Matata kutoka Bagamoyo wakiwa wanatumbuiza nyimbo Nzuri wakati wa kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji Cha maisha Plus
Wakipokea maelekezo kadha wa kadha
MAISHA PLUS/ MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014