Wakazi wa eneo la Mapinga Mkoani Pwani wakiwa kwenye mshangao mkubwa baada ya kushindwa kuvuka Daraja la Mto unaokatisha kwenye eneo hilo baada ya kutokuwepo kwa mawasiliano ya barabara kwa kukatika kwa daraja hilo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini.
Akithibitisha kutokea kwa hitilafu hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Ulrich Matei amesema ni kweli kumetokea kwa tatizo hilo na amewataka watumiaji wa barabara ya Bagamoyo kubadilisha njia na kuwanza kutumia barabara ya Morogoro mpaka hapo daraja hilo litakapofanyiwa matengenezo.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wakati jitihada zikifanyika kurudisha mawasiliano ya barabara na makamanda wakitafakari juu ya kuweka daraja la muda, watu wameanza lawama eti mkandarasi. Lakini ukweli ni mambo ni matatizo yetu wenyewe.
Ukiangalia kati ya hizi picha, kuna moja inaonekana na matete katikati na pembeni yake, kushoto na kulia yanapita maji. Maeneo haya yanayopita maji kwa kipindi fulani yalikuwa yakichimbwa mchanga na kuacha katikati ya mto kuwa na mwinuko.
kiasi kwamba nguzo tatu zinazopitisha umeme mkubwa kwenda Bagamoyo zipo hatarini. Mojawapo maji yanaikaribia zaidi na uwezekano wa kusombwa ni mkubwa kwa sababu miti mikubwa iliyokuwa karibu na eneo hilo nayo imeng'olewa kirahisi kabisa.