Mkuu wa Mkoa wa Dodoma DKT Rehema Nchimbi kitoa maelekezo kwa watendaji hao wakuu wa serikali ngazi za Halmashauri.
Meneja wa Wakala wa Barabara Renald Shimagu akizungumza jambo wakati alipokuwa akifafanua jambo kuusu ujenzi wa barabara uanaoendele mbele ya kamati hiyo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wabunge na wenyeviti wa Halmashauri Mkoani Dodoma wakiwa katika kikao cha ushauri cha mkoa (RCC) kilichofanyika juzi na jana na kutoka na maadhimio mbalimbali.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wiliya ya Kondoa Hamis Mwenda akifafanua jambo wakati alipokuwa akichangia jambo wakati wa kikao cha ushauri cha mkoa wa Dodoma (RCC)
Meya wa manispaa ya Dodoma Emanuel Mwiliko alitoa mchango wake wa mawazo.
Mbunge wa Viti Maarumu Mariamu Mfaki alikutoa mapendekezo yake katika kikao hicho cha siku mbili.
Na John Banda,Dodoma
WABUNGE wa Mkoa wa Dodoma wameshutushwa na baadhi ya kauli za Wajumbe wa Bunge la Katiba za kutaka kuwe na kipengele katika Katiba ijayo cha kuhamishia Makao Makuu ya Serikali kuwa Dar-es-Salaam badala ya Dodoma.
Kauli hiyo ilitolewa na Mbunge wa jimbo la Bahi Omar Badwel kwenye kamati ya ushauri ya Mkoa wa {RCC) alipokuwa anachangia kuhusu maendeleo ya kuhamia makao makuu ya serikali kuhamia Dodoma.
Mbunge huyo ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba alisema hayo kutokana na baadhi ya Wajumbe wa kamati za Bunge kutoa mapendekezo yao na kutaka makao makuu ya Serikali kuyataka yahamie Dar-es-Salaam badala ya Dodoma.
Alisema wajumbe hao wametoa mapendekezo hayo kwa kigezo kuwa toka Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muuungano Mwalimu Julias Nyerere atamke mwaka 1973 kuwa Dodoma iwe Makao Makuu jambo hilo halijatekelezwa mpaka sasa kutokana shughuli nyingi na Wizara nyingi kufanyia Dar-es-Salaam badala ya Dodoma.
Omar alisema kutokana na madai hayo Wajumbe hao wamesema kuwa serikali inaonekama suala hilo ni kama kiini macho kwa Watanzania ambao waliamini kuwa kauri ya Nyerere ingeweza kutekelezwa toka ilipotolewa juu ya kuhamishia Dodoma kama makao makuu ya serikali.
Mbunge huyo ambaye katika kundi lake kuna wabunge wapatao wanne wa Dodoma waliopangwa katika kundi lililopo Dodoma Hotel,na wengine kupangwa kwenye kamati maeneo mengine’
Hata hivyo Wabunge wa Mkoa wa Dodoma wamelipiga suala hilo kwa nguvu zote na kusema kuwa hata kama wajumbe hao watalipitisha wao watalipeleka kwenye kikao cha Bunge kwa ajili ya kuipeleka hoja hiyo ili iweze kujadiliwa na wabunge wote.
Kutokana na suala hilo ambalo liliwashitua baadhi ya wajumbe wa kikao hicho cha ushauri cha mkoa ambacho Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi alikuwa ni Mwenyekiti wake,kwa upande wake alishitushwa na kusema kuwa baadhi ya maeneo ambayo yalitengwa kwa ajili ya kujenga kuwekezwa na serikali kuuzwa.
Dkt Rehema alisema baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa yametengwa kwa ajili ya serikali tayari yamezungushiwa fesi suala ambalo linaloonyesha wazi kuwa uhamiaji wa makao makuu ya serikali utekelezaji wake hauchukuliwi kwa mkazo kama ilivyoamuliwa na serikali.
‘’Oneni wenyewe eneo la ihumwa kuelekea chamwino ambalo lilikuwa maarumu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ambapo eneo hilo lingejulikana kama mji wa kiserikali tayali limeanza kuzungushiwa wigo haliinayoashilia tayali limeuzwa hapa itabidi Mamraka husika watuambie CDA si mpo’’, alihoji Nchimbi
Alisema inawezekana hayo ni maoni yao lakini sisi tunaamini kuwa Dodoma bado ni makao makuu ya serikali mpaka hapo itakavyotolewa kauli nyinginezo za kuyahamisha.