Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

UCHOTAKIWA KUFANYA BAADA YA KUPOKEA BARUA YA KUKATALIWA NAFASI YA KAZI

$
0
0

Wote tunachukia kukataliwa, huwa ni mbaya na tunadhani mtu huyu hakupendi au mwajiri huyu uliyemtegemea hakupendi.Ukiona umekataliwa unaweza kukata tamaa. Baada ya kupokea barua ya kwamba “tunashukuru kwa nia yako ya kufanya kazi katika kampuni yetu, kwa sasa hatutoweza kukuajiri labda wakati mwingine”. Unaweza ukajikuta ukiichukia kampuni hiyo hata watu wa kampuni hiyo na wengine huona aibu hata kuingia kwenye kampuni hiyo baada ya kukataliwa. Hali hiyo inaweza badilisha mwenendo na tabia yako. Hakikisha hali hiyo isikukute wewe.
Hebu tuangalie barua ya kukataliwa yenyewe; 

Je barua ya kutokuajiri au kukukataa inamaanisha nini?
Kama wewe ni miongoni mwa watu waliofanyiwa usaili na ukapita kwenye vikwazo vingi vilivyofuata baadaye katika harakati za kuomba kazi hiyo, inamaanisha unafaa katika nafasi hiyo uliyoiomba. Inamaanisha unafanya vitu vizuri katika harakati zako za kuomba kazi.
Barua ya kukataliwa haimaanishi wewe ni mnyonge au dhaifu, inamaanisha wameshawishika na mtu mwingine zaidi yako katika wale ambao mlikuwa mnashindania nafasi hiyo. Huwezi kujua ilikuwa ngumu kiasi gani kufikia maamuzi hayo, hasa pale ambapo kwenye usaili mlioweza kufika juu mlibaki wachache auwawili tu.

 ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 Lakini iliwalazimu wamchuke mmoja hata kwa kupiga kura. Inamaanisha hata kama mawazo yako yamekuwa hasi kwa jambo hilo, ila wanakuchukulia kama mtu unayefaa sana kwa kazi hiyo.
Fulsa hazijafungwa bado, ila sasa wanakujua vizuri unaweza kuwa mtu ambaye watakuwazia kwenye nafasi nyingine inapotoka. Hivyo unashauriwa kutunza barua zako za kuomba kazi na hata nyaraka zozote zinazohusiana na usaili uliowahi kufanya ili usije anza upya. Na kama kampuni imekutumia barua ya kukukataa hiyo ni dalili kuwa kampuni hiyo inaendeshwa vizuri. Kwa kuwa sasa kutafuta kazi na nafasi za kazi ni adimu. Kama wamefikiria kukutumia barua na wewe usiache kufuatilia nafasi zingine zinapotangazwa kwenye kampuni hiyo.

Je tabia yako inatakiwa iweje?
Kama uliipenda nafasi hiyo ya kazi, haimaanishi kwamba wakikukataa hawataweza kukufikiria kwakati mwingine. Hivyo basi andika barua ya kupokea barua yao na vilevile usiache kuwaambia namna gani ungependa kufanya nao kazi kama watakufikiria wakati mwingine. Na kama una mtu unayemfahamu ndani ya kampuni hiyo, endeleza mawasiliano kana kwamba hakuna kitu kilichotokea au kuathiriwa na kukataliwa nafasi ya kazi.
Onyesha ujasiri wa kukabiliana na hali hiyo, kitu ambacho kitaacha alama kwenye mawazo yao. Fanya kitu sahihi kwa watu sahihi, kukataliwa kazi kusikusababishe ukakata tamaa ya kusonga mbele. Bado unahitajika kufanya mambo makubwa, endelea kuangalia fursa zilizo karibu yako.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>