Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

AJALI YA LORI NA PICKUP YAUA WATU WAWILI

$
0
0
Hii  ndio  pick up uliyogongana  uso kwa  uso la lori  na kusababisha  vifo vya  watu  wawili  usiku wa  leo mjini Iringa
Hili  ndilo  lori  lililogongana  uso kwa  uso  na  pick up eneo la Kibwabwa mjini Iringa na kusababisha  vifo  vya  watu  wawili.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Eneo la  ajali

WATU  wawili  wamefariki  dunia katika  ajali mbaya ya pick up kugongana na  lori  katika  eneo la Kibwabwa  barabara  kuu ya Iringa - Mbeya usiku  wa  kuamkia leo

Kwa  mujibu  wa mashuhuda  ajali  hiyo  imesababishwa  na  dereva wa  gari dogo kuhama  upande  wake na kulifuata  lori hilo kampuni ya Pro-Trans Ltd  ya  jijini Dar es Salaam ambalo  lilikuwa  likitokea  barabara ya  Mbeya  kuja  Iringa na gari  hilo  dogo  lilikuwa  likitokea Iringa  mjini.

Akielezea  tukio hilo mmoja kati ya mashuhuda  John Sanga  alisema  kuwa  wakati ajali  hiyo  ikitokea  alikuwa katika kituo cha Mafuta  kilichopo eneo hilo na kushuhudia  jinsi ambavyo  dereva  wa pick up  hiyo akilifuata  lori hilo kabla  ya  kutokea ajali hiyo mbaya .

Hata  hivyo  alisema  dereva wa  gari hilo  dogo alionyesha  kumfuata  dereva wa  lori  ambapo  dereva  huyo ya  lori alionyesha  jitihada za kumkwepa  bila mafanikio .

Alisema  katika  ajali  hiyo  dereva  alikufa  papo  hapo  huku abiria  wake  alikimbizwa katika  Hospital  ya  Rufaa ya  mkoa  wa Iringa  na kufariki  wakati akipatiwa matibabu 
CHANZO : FRANCIS GODWIN


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>