MAELFU ya wananchi wa mkoa wa Mara pamoja na mikoa jirani wakiongozwa na viongozi wa Serikali,Dini na vyama vya Siasa wameuaga mwili wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara John Gabriel Tupa aliyefariki juzi asubuhi akiwa wilayaniTarime kwa shughuli za kikazi.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa
Kutoka kushoto Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Poul Kasabago,mjumbe wa NEC wa CCM Christopher Gachuma
Mwenyekiti wa Bakwata Musoma mjini akiwa na askofu Msonganzila wa kanisa katoriki
Rais wa klabu za waandishi wa habari Tanzania Keneth Simbeya akitoa salamu za rambirambi
Mtoto wa marehemu aitwaye Gabriel John Tupa akitoa shukurani
Mjane wa baba wa taifa Mwalimu Nyerere alikuwa mmoja wa waombolezaji
Askofu Msonganzila akiweka sahihi kwenye kitabu cha waombolezaji
Mmoja wa waandishi wa habari Nguli Bigambo Jeje akiaga mwili
Baadhi ya waombolezaji wakielekea kuaga mwili wa marehemu
Mwili wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara ukiwa kwenye gari maalumu ukitoka kwenye makazi yake kwenda kanisani
Mwili umepokelewa lango kuu la kanisa katoriki
Mke wa marehemu John Tupa wa pili kutoka kushoto akiwa na wanafamilia kanisani
PICHA NA HABARI KWA HISANI YA SHOMARI BINDA