Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

TBS YAWAFUNDA WALEMAVU WASIOSIKIA (VIZIWI) KUTOKA MIKOA YA DODOMA,SINGIDA, TABORA NA SHINYANGA JUU YA UZALISHAJI WA BIDHAA KWA KUZINGATIA VIWANGO VYA UBORA

$
0
0
Meza kuu ikiongozwa na Mkuu wa mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi wakiwashangilia kwa lugha ya alama wajasiriamali wenye ulemavu wa kusikia (hawapo pichani) wakati wakijitambulisha kwenye semina iliyoandaliwa na TBS kwa ajili ya kuwafunda walemavu hao masuala ya viwango vya ubora  katika shughuli za,uzalishaji.
Mkuu wa mkoa Dodoma Dr Rehema Nchimbi akiwasisitizia walemavu wasiosikia (viziwi) kuzingatia ubora wa viwango kwenye bidhaa wanazozalisha kwenye sekta ya kilimo, ufugaji nyuki na mifugo na ujasiriamali ili kunufaika na masoko ya kimataifa wakati akifungua semina kwa walemavu hao juu ya masuala ya ubora wa viwango  iliyoandaliwa na shirika la viwango tanzania TBS, semina hiyo ilifanyika leo mjini Dodoma, wengine pichani ni maafisa kutoka TBS.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 Afisa uhusiano wa taasisi ya maendeleo ya viziwi tanzania  ndg. Nicholaus Lubinga (aliyesimama nyuma) akizungumza jambo kwa lugha ya alama wakati wa semina  ya masuala ya viwango vya ubora kwa wwjasiriamali wenye ulemavu wa kusikia iliyoandaliwa na TBS ambayo imefanyika mjini dodoma.
 Wajasiriamali wenye ulemavu wa kusikia viziwi wanaojihusisha na shughuli za uzalishaji katika sekta za kilimo, mifugo na nyuki na ujasiriamali kutoka mikoa ya Dodoma singing, tabora na shinyanga wakisikiliza kwa makini hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na mkuu wa mkoa Dodoma na kutafsiriwa kwa lugha ya alma wakati wa ufunguzi wa semina ya masuala ya ubora wa viwango iliyoandaliwa na shirika la viwango tanzania TBS na kufanyika mjini Dodoma.
 Baadhi ya wajasiriamali wenye ulemavu wa kusikia (viziwi) wanaojihusisha na shughuli za uzalishaji katika sekta za kilimo, ufugaji mifugo na nyuki na ujasiriamali kutoka mikoa ya Dodoma, singida, Tabora na shinyanga wakishangilia hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na mkuu wa mkoa Dodoma na kutafsiriwa kwa lugha ya alama kwenye semina ya masuala ya ubora wa viwango iliyoandaliwa na shirika la viwango tanzania TBS mjini Dodoma.
Picha ya pamoja baina ya mkuu wa mkoa wa dodoma Dr. Rehema Nchimbi, wataalamu wa masuala ya viwango vya ubora kutoka TBS na walemavu wasiosikia (viziwi) kutoka mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na Shinyanga muda mfupi baada ya mkuu huyo wa mkoa kufungua semina kwa walemavu hao juu ya  masuala ya ubora wa viwango iliyoandaliwa na shirika la viwango tanzania TBS na kufanyika mapema siku ya  Jumatatu Machi 24, 2014.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>