Kama unatafuta kufanya zaidi ya kucheza michezo ya kwenye simu hizi za kisasa *smart phones* kuna programu nyingi zipo na zinaendelea kuja kuongeza uwezo wako wa kufanya kazi. Zipo nyingi ukianza kuzitafuta utatumia muda mwingi sana, ndio maama tumekuchagulia chache na jinsi zinavyoweza kukusaidia, jaribu hizi tano na hutaweza jua kwanini uliweza kuishi bila kuwa nazo?
1. Dropbox (Bure)
Dropbox ni programu ambayo inakusaidia kutunza vitu kama picha, filamu, na hata mafaili yako huko hewani na unaweza kuyatumia mara tu unapoyahitaji wakati wowote na mahala popote endapo tu utakuwa na simu yenye intaneti au kompyuta yenye intaneti . Unaweza kuambatanisha mafaili au picha na kuzipata sehemu yeyote kwenye imu au kompyuta bila kutumia barua pepe. Na Programu hii inakusaidia kwamba hata kama kompyuta yako au simu imeharibika au kuibiwa ni rahisi kupata vitu vyako bila shida wala wasiwasi wowote.
2. TripIt (Bure)
TripIt inakusaida kupangilia safari zako, unachotakiwa kufanya ni kila email ya safari au taarifa za safari kuzipeleka kwa TripIt hivyo kukusaidia kujua lini utakuwa wapi na kukuwezesha kuwasiliana na watu ambao unataka wajue taarifa zako za safari kupitia Facebook au Linkedin na vilevile kukuonyesha ramani ya kule unakokwenda na kukwonyesha mpangilio wa mji na aina ya usafiri wa mahali hapo.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
3. Abukai Expenses ($39 / kwa mwaka)
Kama wakati wote unatakiwa kuandika ripoti ya matumizi yako na kufanya madai ofisini na unajua ni jinsi gani inauma kama ulifanya matumizi ya kiofisi kwa hela yako halafu umepoteza risiti. Abukai Expenses inakutengenezea ripoti ya matumizi yako kwa picha ya risiti. Unachotakiwa kufanya ni kuipiga picha ile risiti kabla ya kuiweka popotena Abukai itamalizia kila kitu.
4. Zoho Invoice ($15 / kwa mwezi)
Kutengeneza, kujua na kumpelekea mteja risiti au kudai malipo ni kitu ambacho kinasumbua biashara ndogo. Zoho Invoice inakusaidia na kufanya kazi yako iwe rahisi bila ya wewe kumlipa mhasibu gharama za kufanya kazi hiyo kama makampuni makubwa. Ingawa kuna programu nyingi tu za bure kukusaidia kuendesha biashara yako na kujua fedha zinakwendaje, watu gani unawadai na watu gani wanakudai. Kama una smart phone, hiyo ni zaidi ya simu itumie vizuri kuendeleza biashara zako na kazi zako.
5. Pulse News (Bei yake ni Bure)
Pulse inakusaidia kukusanya habari kutoka vyanzo tofauti tofauti unavyovipenda kwa wale ambao hawana muda wa kusoma. Programu hii inakusanya habari hizo na kuzitunza kwenye simu yako ili uweze kuzisoma baadaye wakati hauko kwenye intaneti. Nikama kuwa na gazeti kwenye simu yako.
Hivyo utendaji wako unaweza kusaidiwa na programu nyingi ambazo zinakuja kutokana na teknoloJia, fanya uchunguzi halafu chagua kitu kitakachokusaidia kufanya kazi sawa sawa na kwa ustadi mkubwa kwa kutumia simu yako. Dunia tuliyopo ni tofauti sana na ya miaka kumi iliyopita hivyo jitahidi kwenda na wakati.