Mchezaji wa Swansea City Sung-Yueng Ki akipongezwa na wachezaji wenzake mara baada ya kuiandikia Timu yake ya Swansea Goli la Kwanza katika Mchezo wa Kwanza wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya timu ya Man U katika Dimba la Old Traford ambapo Man U imekubali Kichapo cha Goli 2 Kwa 1
Mchezaji wa Man U akijaribu kutoa Pasi kwenye Mchezo wa Kwanza wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Swansea katika Dimba la Old Traford huku Man U wakikubali kichapo cha Goli 2 kwa 1
Nahodha wa Man U Wayne Roone akiwania mpira na Mchezaji Williams Kutoka Swansea katika Mchezo wa Kwanza wa Ligi kuu ya Uingereza uliochezwa leo katika Dimba la Old Traford na Swansea Kuibuka Kinara kwa kuitandika Man U goli 2 kwa 1
Hatari langoni Mwa timu ya Man U katika mchezo wa Ligi kuu ya Uingereza uliochezwa leo huku Man U ikikubali kipigo cha Magoli 2 kwa 1 Nyumbani
Sung- Yueng Ki mchezaji wa Swansea aliyeiandikia timu yake Goli la Kwanza katika Mchezo wa Ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Man U, huku Man U ikikubali kupokea Kichapo cha Magoli 2 kwa 1 Nyumbani.
Nahodha Wa Man U Wayne Roone Akishangilia goli la Kusawazisha ambalo lilipelekea Timu yake kuwa sare katika Dakika ya 53 ya Kipindi cha Pili. Hadi dakika ya Mwisho Man U ikakubali kipigo cha Goli 2 kwa 1 na Swansea kuibuka Mbabe
Wayne Roone akiifungia Goli la kufutia Machozi timu yake katika Mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Uingereza iliyoanza rasmi leo huku Man U ikipokea kichapo bila kupenda nyumbani dhidi ya Swansea
Kocha Mkuu wa Man U, Louis Van Gaal akishangaa kilichotokea wakati wa mechi ya Ligi kuu ya Uingereza huku Kocha Msaidizi Ryan Giggs akistahajabu kwa alichokiona kwa timu yake kupokea kipigo bila wao kuamini cha Magoli 2 kwa 1 dhidi ya Swansea. Picha Kwa Hisani ya BPL